Msanii wa muziki wa
Hip Hop, Bill Nas amelazimika kusitisha kwa muda shughuli za muziki wake ili
kuweka mambo sawa katika chuo anachosoma.
Rapper
huyo ambaye anabukua katika chuo cha College of Business Education (CBE) jijini
Dar es salaam amepata supplement tatu katika baadhi ya masomo yake.
Akiongea
na meneja wa rapper huyo, Mchafu Chakoma amesema Bill Nas wiki hii
atakuwa busy kwa ajili ya maandalizi ya kufanya supplementary zake.
“Bill
Nas wiki anahitaji muda mwingi wa discussion kwa ajili ya supp zake, amepata
supp tatu na baada ya wiki moja atarudi kwenye mishe za muziki,” alisema
Mchafu. “Yaani hajapata maksi ambazo zilikuwa zinahitajika katika hayo masomo
yake, anatakiwa kupata maksi zaidi ya 40, sasa amepata chini ya hapo kwa hiyo
amelazimika kurudia mitihani,”
Chakoma
amesema yeye kama meneja wa LFLG, atahakikisha Bill Nas anaendelea kufanya
vizuri katika masomo na muziki.
“Mimi
nimeanza kumsaidia Bill Nas hata kabla hajaanza muziki, kwa hiyo wakati anasoma
ndo akaniambia broo nataka kufanya muziki, mimi nikamwambia kama unaweza poa,
na wakati anaanza hatukuwa tunafanya muziki kama biashara kwa sababu tunajua
kijana bado anasoma,” alisema Chakoma.
No comments:
Post a Comment