Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Rodson amelithibitishia gazeti hili
kutokea kwa matukio hayo juzi jioni.
Hata hivyo, alisema kuwa asingeweza
kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu alikuwa kwenye sherehe za uzinduzi
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Geita.
Hata hivyo, habari za uhakika
kutoka katika Kitongoji cha Elimu, Kijiji cha Kaseme kilichopo wilayani Geita
ambako mwinjilisti huyo alikuwa akiishi na familia yake zinasema kuwa alichukua
uamuzi wa kumwadhibu binti yake huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu,
baada ya kumkuta akizungumza na mwanamume ambaye hata hivyo hakufahamika.
Inaelezwa kuwa baada ya kumpiga,
alimchukua na kwenda naye nyumbani na kumfungia ndani huku akiendelea
kumwadhibu hadi alipofikwa na umauti.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakuwa
tayari kutajwa jina gazetini, baada ya mwinjilisti huyo kubaini kuwa amemuua
mwanaye, alichukua uamuzi wa kukimbia umbali ya kilometa moja na kujitundika
mtini kwa kamba iliyomnyonga hadi kufa.
Kamanda Mponjoli, alisema kuwa
uchunguzi wa Polisi na wa madaktari unaendelea na kwamba utakapokamilika miili
ya marehemu wote wawili itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
Aliitaka jamii kuwa makini wakati
wa kuadhibu watoto kwa kuwa si wakati wote wanapaswa kupewa adhabu kali na
hatarishi kama vipigo vinavyoweza kuwasababishia umauti.
Wakati huohuo, baadhi ya wakazi wa
Kata ya Kaseme wanaomfahamu mwinjilisti huyo walieleza kwa nyakati tofauti
kushangazwa na hatua aliyoichukua kwa sababu hakuwa na tabia ya uhalifu wa aina
yoyote wala ukatili.
Masaga Makanika na Magesa Masai
kila mmoja kwa wakati wake alisema kuwa mwinjilisti huyo alikuwa ni muumini
mzuri wa dini asiye na rekodi mbaya ya matukio ya kiuhalifu na kwamba hatua
alizochukua zimewaacha na maswali mengi huku wakifikiri kuwa pengine ni mipango
ya Mungu au majaribu ya shetani.
No comments:
Post a Comment