
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo
amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.
Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja
amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na
Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.
Alisema baada ya kupata ajali hiyo
walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia
kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguzi alisema
hakuumia popote ni wazima.
Alisema baada ya hapo Waziri na watu
waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge.

Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.

Askari wa usalama barabaran wilayani Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea

No comments:
Post a Comment