
Watumiaji wa smartphone au maarufu
Simu-Janja ni watu makini sana linapokuja suala la ukubwa wa simu, mwenendo wa
masoko kwa sasa unaonyesha wanunuaji wengi wa simu wanavutiwa sana simu zenye
kioo kipana.
Lakini sio wapenzi wote wa simu
wanatamani simu zenye kioo kipana, watumiaji wengine wanapenda simu zenye
ukubwa wa wastani. Fununu zilizotapakaa ni kuwa TECNO wanakuletea simu mpya
Phantom 6 ambayo pia itakuja na matoleo mengine kama Phantom 6 Plus na Phantom
6 mini.
Fununu hizi zinaweka wazi kwamba
watengenezaji hawa wakubwa wa simu za mkononi wana mkakati kabambe wa kuwavutia
watumiaji wakubwa wa simu kununua matoleo haya mapya yanayotarajiwa kutoka
Septemba hii pindi TECNO Phantom 6 itakapazinduliwa.
HAKUNA SHAKA JUU YA UKUBWA WAKE
Jambo hili linatia moyo huku TECNO
ikiwekwa bayana katika uvumi unaosambaa angalau kwa vidokezo na muonekano ambao
unasemekana ni rasmi Tecno Phantom 6 itaboreshwa zaidi na wala haitopunguziwa
sifa zake kuu.
Nafikiri hili ni jambo la
kufurahisha sana kwa sababu mara nyingi tumekuwa tukiona makampuni mengi ya
simu yakiwauzia wateja wao simu zenye uwezo mdogo katika maduka yao makubwa
wakitumia jina la makampuni yanayobamba kwa kuuza simu. Watumiaji wengi wa simu
siku hizi wako makini sana na hawadanganyiki kirahisi.
PHANTOM 6 NA MATOLEO MAPYA YA TECNO
YATAKUWA NI GUMZO?
Watengenezaji hawa wakubwa wa simu
za TECNO wamekuwa wakipambana kuweka toleo lao bora kabisa kwenye mauzo kuanzia
Phantom A+ mpaka Phantom Z au Z mini, Phantom 5 na sasa Phantom 6. Swali
linalobaki ni je, phantom 6 itabadilisha mtazamo wa baadhi ya wananuaji wa
simu?
Unadhani wpenzi wa Smartphones
wataanza kuiona Phantom 6 kama moja ya toleo la kipekee kama inavyotarajiwa na
wengi? Na inasemekana kuwa Phantom 6 ama 6 + itakamata soko kubwa kipindi hiki
endapo toleo zitambulishwa kwa upekee kwa wakati muafaka.
Mbali na fununu zote hizi
tunasubirri kuona toleo rasmi la Phantom 6 kuzinduliwa ifikapo Septemba.
Endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno
kama ilivyoorodheshwa hapa chini.
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ
No comments:
Post a Comment