Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewataka wananchi
kuwatenga wasanii wa kike ambao wanavaa nguo ambazo zinaacha sehemu zao za
mwili wazi.
Akijibu
swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mery Mwanjelwa (CCM) Jumanne
hii kuhusu ushiriki wa viongozi wa dini pamoja na jamii katika kulinda sanaa
ili itumike vizuri bila kumzalilisha mwanamke, Nape amesema kila mtanzania ana
haki ya kulinda hadhi ya mwanamke.
“Wizara
yangu inatoa wito siyo tu kwa viongozi wa dini, hawa wasanii wetu wamo katikati
ya jamii zetu, hawa wasanii ni watoto wetu, ni ndugu zetu, wanaingia kwenye
nyumba mbalimbali za ibada na kukutana na viongozi wetu wa dini, natoa wito kwa
kila mmoja wetu aone kwamba kuna umuhimu wa kila mmoja kushiriki na
kuwahamasisha wasanii wetu wanazingatia maadili ya Tanzania sana katika
shughuli zao za sanaa,” alisema Nape. “Nataka nilihakikishie mbunge lako
mweshimiwa spika ikiwa jamii itayakataa matendo yanayofanywa na wasanii, wasanii
hawa wataacha haya matendo lakini ikiwa jamii itayashabikia nakuyapenda wasanii
hawa wataona ndio fashion na wataendelea kuyafanya kwa hiyo hata kama sisi
tukihamasisha namna gani, kama jamii haitayakaa na kuyaona hayafai kila
mtanzania ataona mwanamke akidhalilishwa amedhalilishwa mzazi wake,
amedhalilishwa ndugu yake, haya matendo yatakoma katika jamii yetu, nadhani ni
swala jamii zaidi kuyakataa na kuwatenga kijamii wale ambao wanafanya shughuli
za kuwadhalilisha akina mama wetu,”
Pia
Nape alisema mpaka sasa kuna wasanii wawatu wa kike ambao walifungiwa kutokana
kufanya shughuli za sanaa kinyume na maadili.
No comments:
Post a Comment