Muongozaji wa video
nchini, Nisher amedai kuwa amelazimika kuwa kimya makusudi ili kujiandaa kuja
na ujio wa awamu nyingine akiwa na nguvu zaidi.
Muongozaji
huyo wa Arusha ameiambia Bongo5 kuwa hapendi tena kufanya mambo kawaida, bali
kuja na kitu chenye kishindo cha kutisha.
“Right
now I’m taking my time kidogo,” amesema Nisher kueleza kwanini ghafla amekuwa
kimya tena. “I’m coming out with something big, ila nipo kwenye, so sio kitu
cha haraka. Kwa upande wangu right now, I’m not about releasing kazi kila
siku,” amesisitiza.
“I’m
all about big moves basi. I do something big na chill nafanya mambo mengine na
return na hit zingine na chill sababu kwa sasa nina mambo mengi sana kwenye
sahani yangu, na kujigawa sana inakuwa kazi so na balance,” ameongeza.
Hivi
karibuni pia Nisher alifuta picha zote kwenye akaunti yake ya Instagram.
No comments:
Post a Comment