Dayna Nyange amedai kuwa kupitia jukwaa la Fiesta mwaka la huu amefahamu
nyimbo zake zinazopendwa na mashabiki wake wa mikoani.
Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa, steji ndio kipimo
chake cha kuwajua mashabiki wake na kuwa karibu nao.
“Kikubwa nimefahamu ninavyokuwa kisanaa maana ni tamasha
kubwa na nakutana na watu wengi. ‘Nivute Kwako’, ‘Ido’, ‘Komela’ na ‘Angejua’
zote zinapendwa na mashabiki wa mikoani,” amesema Dayna.
Msanii huyo ameongeza kuwa video ya wimbo wake ‘Komela’
aliomshirikisha Bill Nas imechelewa kutokana na kuingiliana kwa vitu ila
amewataka mashabiki wake waendelee kuisubiria kwa kuwa maandalizi yote yapo
tayari.
No comments:
Post a Comment