Baadaye, imebainika kwamba ilikuwa
ni sigara ya kisasa ifahamikayo kama 'e-cigarette'.
Waandamanaji kadha wamejitokeza
katika barabara za El Cajon, viungani mwa mji wa San Diego, kulalamikia kuuawa
kwa Alfred Okwera Olanfo, aliyekuwa na umri wa miaka 38.
Bw Olango aliuawa Jumanne baada ya
polisi kujibu wito kutoka kwa dadake Olanfo ambaye aliitisha msaada.
Aliwaambia maafisa wa polisi kwamba
kakake alikuwa anaugua ugonjwa wa kiakili.
Mkuu wa polisi wa El Cajon Jeff
Davis amesema Bw Olango alifariki baada ya kupigwa risasi na afisa mmoja.
Polisi mwenzake alifyatua risasi za mipira za kumtuliza.
Polisi wamekiri kwamba kifaa
alichokuwa nacho hakikuwa silaha.
Badala yake, wamesema alikuwa na
sigara ya rangi ya fedha ya urefu wa inchi tatu (7.6cm).
Agnes Hassan, rafiki wa familia ya
Bw Olango, anasema alimfahamu mwanamume huyo, ambaye anasema alikuwa na elimu
nzuri lakini alikuwa na matatizo ya kiakili.
Bi Hassan anasema alikaa na Olango
kwa muda katika kambi ya wakimbizi wakielekea Marekani.
Mtaa wa El Cajon, San Diego huishi watu karibu
100,000 na una idadi kubwa ya wakimbizi, wengi ambao walikimbia vita Iraq na
Syria
No comments:
Post a Comment