Kiongozi huyo wa umri wa miaka 72
amekuwa madarakani tangu 2004 na chama chake kimetawala taifa hilo la visiwa
kwa miongo minne.
Alifanya tangazo hilo la ghafla
kupitia runinga siku ya Jumanne ambapo aliahidi kuondoka madarakani ifikapo 16
Oktoba.
"Baada ya kuhudumu miaka 12
kama rais, wakati wangu kukabidhi madaraka kwa kiongozi mpya umewadia. Kiongozi
mpya atafikisha Ushelisheli hatua hiyo nyingine ya ufanisi."
Aprili, bunge la nchi hiyo
liliidhinisha marekebisho ya katiba na kupunguza muda wa rais kuongoza kuwa
mihula miwili ya miaka mitano badala ya mihula mitatu ya miaka mitano.
Mrithi wake atakuwa makamu wa rais
wa sasa Danny Faure, 54, ambaye amehudumu katika wadhifa huo tangu 2010.
Atalishwa kiapo 16 Oktoba na
kuongoza kipindi kilichosalia cha muhula wa sasa wa Michel.
Muungano wa vyama vya upinzani wa
Seychellois Democratic
Alliance ulishinda viti vingi
kwenye uchaguzi uliofanyika 8-10 Septemba katika taifa hilo la visiwa 115.
Upinzani ulipata viti 15 nacho
chama cha upinzani cha Parti Lepep kikashinda viti 10.
Upinzani umeahidi kufanya kazi na
rais kwa maslahi ya taifa.
Parti Lepep kimekuwa madarakani
tangu 1977, mwaka mmoja baada ya uhuru, na kimeshinda uchaguzi tangu kurejeshwa
kwa siasa za vyama vingi 1993.
Michel alikuwa tayari amehudumu
mihula miwili ya miaka mitano mitano na alikuwa ameanza kuhudumu muhula wa tatu
Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment