Abdi Asis alikuwa akifanya kazi
kwenye radio moja binafsi iitwayo Shabelle ambayo wafanyakazi wake awali
waliwahi kulengwa na mashambulizi
Mwandishi wa habari huyo ambaye
amefanya kazi na Radio Shebelle kwa miaka kadhaa alipigwa risasi na watu wawili
wenye silaha wakiwa na pikipiki mjini Mogadishu na kupoteza maisha.
Uongozi wa Redio aliyokuwa
akifanyia kazi umethibitisha kifo chake na kusema watu wenye silaha walitoweka
kwenye eneo la tukio,hii si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari wa Redio
Shabele kuuawa kwa kupigwa risasi nchini Somalia.
Umoja wa Mataifa hivi karibuni
ulitoa ripoti ikiiorodhesha Somalia kuwa miongoni mwa nchi hatari kwa waandishi
wa habari kufanya kazi. Ripoti zao zinasema kati ya mwezi agosti mwaka 2012
mpaka june 2016, waandishi wa habari 30 waliuawa nchini Somalia.
Ripoti hiyo inasema karibu waandishi
wa habari 120 wamekamatwa na wanashikiliwa kati ya januari mwaka 2014 na Julai
mwaka 2016
No comments:
Post a Comment