Serikali ya mkoa wa Dodoma imeahirisha mapokezi ya Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa yaliyokuwa yafanyike leo hadi hapo vikao vya Bunge vinavyoanza Jumanne
wiki ijayo vitakapomalizika.
Akizungumza jana Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana
alisema mkoa unajipanga namna ya kumpokea Waziri mkuu baada ya vikao hivyo
kumalizika na hivyo.
Aidha Rugimbana alisema ujio wa Waziri Mkuu mjini humo
bado uko palepale na kwamba maandalizi ya namna ya kumpokea yanaendelea.
Kamati za Bunge 12 zimekuwa zikiendelea na vikao vyake
mjini Dodoma kwa wiki ya pili mfululizo. Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Dodoma
Mjini, Christina Mndeme, alisema Waziri Mkuu angepokelewa katika eneo la
Mtumba, kisha kuzungumza na wakazi wa Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri.
Uamuzi wa kuhamia rasmi Septemba Mosi ulitangazwa na
Waziri Mkuu mwenyewe katika maadhimisho ya siku ya mashujaa Julai 25 mwaka huu
yaliyofanyika mjini hapa.
CHANZO: MWANANCHI
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment