Msanii na mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, Barnaba Classics
amesema pesa zikimtembelea atajenga kanisa.
Muimbaji
huyo ambaye pia huwaandikia wasanii nyimbo za gospel, alisema hawezi kuwa
muhubiri bali atafanya issue tofauti ambazo zitampendeza mwenyezi mungu.
“Mimi siwezi kuja kuwa muhubiri ila
nikija kupata hela kupitia muziki nimepanga kuja kutengeneza kanisa ili liweze
kutoa huduma kwa wanaumini ila si kuhubiri kanisani kama ambavyo shabiki wangu
alivyosikia huko mitaani,” Barnaba alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA
Radio.
Mbali na hilo msanii huyo alisema
kuwa kwa sasa yeye hana muda wa kumfundisha mtu jinsi ya kuimba bali anaweza
kumpiga msasa mtu ambaye tayari anaweza kuimba kwani yeye muda wa kumfundisha
mtu kwa sasa hana.
“Mimi saizi kiukweli sifundishi mtu
namna ya kuimba kwani sina muda wa kufundisha mtu ila kama mtu unakipaji naweza
kukupiga msasa ukafanya vizuri ila si kufundisha mtu” alisema Barnaba
No comments:
Post a Comment