
Watu 10 wamefariki dunia na wengine
44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Barcelona walilokuwa wakisafiria
kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Lindi kupata ajali eneo na
Miteja mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata
Mzinga imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande
wa kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva
alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.
Pia Kamanda Mzinga amesema kuwa
wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa basi hilo lilikuwa na uwezo wa
kubeba abiria 48, wakati basi hilo linapata ajali kulikuwa na abiria 54 kitu
ambacho ni kosa kisheria.
Aidha, Kamanda Mzinga amesema kuwa
bado wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini alipo dereva ili kuweza kufahamu
ni kipi hasa kilichotokea. Hadi sasa wanamshikilia kondakta wa basi hilo lakini
bado hajaweza kuelezea tukio halisi.


No comments:
Post a Comment