Inafuata kuongezeka kushuhudiwa
ghasia katika miezi ya hivi karibuni na wasiwasi unoaongezeka katika mji mkuu
Juba, licha ya kuidhinishwa makubaliano ya amani mwaka jana.
Shirika hilo la kimataifa la
kutetea haki za binaadamu, linasema ahadi inayoungwa mkono na waziri wa mambo
ya nje wa Marekani John Kerry na viongozi wengine wa kieneo pamoja na pande
mbili za mzozo kuidhinisha mahakama maalum, imekwama.
Linasema ukiukaji wa sasa
uliosababisha maelfu kuuawa, wanawake kubakwa, na vijiji kuharibiwa ni mambo
yanayopasa kutoa shinikizo jipya katika kufanikisha kuundwa mahakama hiyo
maalum.
Takriban miaka mitatu baada ya kuzuka ghasia katika
taifa jipya Afrika, zilizowalazimisha watu milioni 2.6 kuyatoroka makaazi yao,
na kusabaisha vifo vya maelfu huku wengine wakijeruhiwa, Amnesty International
linaonya kuwa ahadi ya kuidhinishwa mahakama hiyo maalum imepuuzwa.
Makubaliano ya amani yalioitiwa
saini mwaka jana kati ya rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake, Riek Machar
yalitoa ahadi ya kuidhinisha mahakama maalum kusikiza tuhuma za uhalifu wa
kivita ikiwemo mauaji na ubakaji.
Wakati Sudan kusini sio mwanachama
wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, pendekezo ilikuwa ni kuunda mahakama
hiyo itakayojumuisha mahakimu wa nchini na wa kimataifa ambayo iwapo itabidi,
makaazi yake yatakuwa nje ya nchi ya Sudan Kusini.
Kundi hilo la kutetea haki za
binaadamu linasema maovu yanayotuhumiwa ambayo Muungano wa Afrika tayari
imenukuu 'ni lazima haki itetendeka' na kusema mahakama hiyo haitoshughulikia
ukiukaji wa haki za binaadamu lakini pia ni muhimu katika 'nguzo ya kufikia
amani ya kudumu'.
Amnesty linasema kesi ya hivi
karibuni dhidi ya aliyekuwa rais wa Chad, Hissene Habre kwa uhalifu wa kivita,
iliyosikizwa katika mahakama ya Afrika, inapaswa kuwa kama kichochezi cha
kuwawajibisha viongozi wa Sudan kusini.

No comments:
Post a Comment