Mtandao wa Facebook umeanzisha mfumo mpya wa mtandao mpya uliopewa jina
la ‘Work Place’ ambao utasaidia makampuni kurahisisha mawasiliano kwa njia ya
ujumbe wa video ya moja kwa moja.
Mfumo
huo mpya umebuniwa na mtandao huo kwa ajili ya kuleta ushindani kwa mifumo
mingine ya mawasiliano iliyopo kama Email na mingine.
Mfumo wa mawasiliano wa ‘Worl
Place’ utaingia kwenye masoko mengine sawa na ule wa mtandao wa Microsoft wa
Yammer ambao makampuni yanaweza kutumia sawa na ule wa Slack ambao ni wa
mawasiliano ya ujumbe.
Facebook imekuwa ikiufanyia majaribio mfumo huo mpya
ambao awali ulipewa jina la ‘Facebook at Work’ kwa muda wa miaka miwili na
mpaka sasa zaidi ya makampuni 1000 tayari yanautumia

No comments:
Post a Comment