
Ukimwaga mboga wenzio wanamwaga ugali. Ukweli wafahamika
baada ya mara kadhaa rapper Young Dee kukanusha kuwahi kuwa na mahusiano na
video vixen kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Amber Lulu.
Akiongea
na U-Heard ya Clouds FM, Amber Lulu amefunguka ukweli kwa kusema kuwa amekuwa na
mahusiano na rapper huyo kwa tangu miaka minne iliyopita wakati akiwa mkoani
Mbeya.
“Marafiki zangu wanajua ni jinsi
gani nilivyokuwa naishi naye, mara ya mwisho alikamatwa na polisi mimi ndio
nilienda kumtoa ndugu zake wote walikataa kwenda, Mimi nimeenda. Matatizo yangu
yeye anayafurahia ina maana. Sikuwa nimefanya vile kwa kuwa alikuwa ni mpenzi
wangu ni mtu ninayemfahamu siku nyingi na ambaye tupo wote,” amesema Amber.

No comments:
Post a Comment