Hatma ya ‘East Coast Team’ ipo mikononi mwa King Crazy GK - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday 6 October 2016

Hatma ya ‘East Coast Team’ ipo mikononi mwa King Crazy GK

       gk
Mkali wa wimbo Zigo na member wa ‘East Coast Team’ Ambwene Yessaya ‘AY’ amesema King Crazy GK ndiye mwenye maamuzi wa mwisho ya nini kifanyike kwenye kundi la ‘ECT’ ambalo lilijizolea mashabiki wengi katika kipindi cha nyuma.

Rapper huyo amesema uwezekano wa kundi hilo kurudi upo lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni King Crazy GK ambaye amemtaja kama Amiri Jeshi mkuu wa kundi hilo.
“Kwanza East Coast Team ipo, ni kwamba mimi na FA tulitoka kufanya kazi zetu binafsi, ila kufanya kazi sisi wote watatu itatokea lazima tuifanye, kwa hiyo ni upande wake (GK) kuamua kwa sababu yeye ndiyo Amiri Jeshi mkuu, East Coast ilikuwepo na ipo, siyo kwa vile AY na FA wametoka”, AY alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Pia rapper huyo amepongeza ujio mpya wa GK kupitia wimbo wake aliyoachia hivi karibuni.

“Nimeona amefanya comeback ya kwake na amejitahidi kwa uwezo wake, ameswitch na yuko sawa, mimi na GK tunashirikiana katika njia tofauti tofauti nje ya muziki pia”, alisema AY

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here