
Kim Kardashian anadai kuwa ameathirika tena, awamu hii na tovuti ya
udaku iliyoripoti kuwa alidanganya kuvamiwa na watu wenye silaha na kuporwa,
kisha kutaka alipwe bima ya mamilioni ya dola kwa mali alizopoteza.
Kwenye
kesi hiyo iliyofunguliwa Manhattan Jumanne hii, Kardashian, 35, anasema
MediaTakeOut.com iliandika habari ya kumchafua yenye kichwa cha kupotosha kuwa
alikuwa muongo na mwizi kwa kutengeneza tukio hilo.
Maelezo yenye kurasa nane ya
shitaka hilo, yanadai kuwa licha ya maisha yake kuwa hatarini, Kim amekuja
kuumizwa zaidi na taarifa hiyo kuwa alipanga kila kitu.
“Kardashian was assaulted and
robbed by two masked men, who placed a gun to her head, duct-taped her hands,
legs and mouth, and then left her lying helplessly on the bathroom floor of her
rented apartment while the thieves absconded with millions of dollars in
jewelry,” yamesema maelezo.
Habari ya tovuti hiyo imesema Kim
alitengeneza kisa hicho ili kutengeneza kiki ya show yake ya TV. Media Take Out
inadaiwa kukataa kuifuta habari hiyo na imegoma kumuomba radhi.
Kim anataka mmiliki wa tovuti hiyo
Fred Mwangaguhunga kumlipa kiasi kisichojulikana cha fedha kwa madhara
aliyoyapata.
Credit
BBC

No comments:
Post a Comment