Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi
akikabidhiwa Mabati bando 20 na Mkurugenzi wa kampuni ya MUYA INVESTMENT
Jua Kali Mkono kwenye ujenzi wa shule ya msingi Bwawani.
WANANCHI wa kitongoji cha njia panda
kata ya Ludete wilaya na mkoa wa Geita wamesema kuwa kujengwa kwa shule ya
msingi Bwawani kutasaidia kupunguza ajali za barabarani kwa
wanafunzi ambao walikuwa wakitembea umbali wa mrefu kufuata elimu.
Hayo wameyasema wakati
wa kupokea msaada wa mabati bando 20 zenye thamani ya sh.milioni 5.8
yaliyotolewa na kampuni ya( WUZHOU INVESTMENT COMPANY LTD)
ambao wanaojihusisha na uuzaji wa pikipiki aina ya San LG pamoja na
vipuri .
Wananchi wamesema kuwa kujengwa
kwa shule hiyo kwenye kata yao pamoja na kampuni hiyo kuchangia mabati
kutasaidia watoto kuacha kutembea umbali mrefu hali iliyokuwa inasababisha vifo
wakati wa kuvuka barabara kwa watoto pindi waendapo shuleni.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mtendaji
wa kata ya Ludete Aloyce Kamuli ameeleza kuwa pamoja na zoezi la kuendelea
kujenga shule ya msingi ya Bwawani lakini bado wanachangamoto kubwa zaidi ya
kukosekana shule ya sekondari katika kata hiyo hali ambayo imekuwa ikisababisha
wanafunzi waliopo katani hapo kutembea umbali wa kilomita nyingi kufata elimu.
Akikabidhi msaada huo msemaji wa kampuni
ya muya investment kanda ya ziwa Rashid Hasan amefafanua kuwa lengo
la kutoa mabati hayo ni kuunga jitihada za Raisi John
Magufuli za kuinua elimu nchini na kupambana na changamoto ambazo
zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika shule zilizopo nchini hapa.
Wakati huo huo meneja wa kampuni ya
uchimbaji wa dhahabu ya ANDLU GOLDEN AND PATINZI Kurwa Sagwea amekabidhi
sh milioni 2 kwa ajili ya madawati katika shule ya msingi Subola kata ya kaseme huku
mkuu wa shule hiyo Steven Kibiliti akielezea kuwa bado wanakabiliwa
na changamoto kubwa ya upungufu wa madarasa shuleni hapo.
Akipokea misaada hiyo mkuu wa wilaya ya
Geita Hermani Kapufi amepongeza makapuni hayo na kusema kwamba kwa kutoa msaada
wao kwa moyo wanajiwekea hadhina mbinguni na kuwataka wengine kuiga mifano ya
kuchangia maendeleo yao kwenye maeneo wanayoishi.

No comments:
Post a Comment