Donald Trump ametangualia kwa
kutetea matusi aliyotoa kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu za siri kwa
kumshambulia Hillary Clinton na mumewe.
Mgombea huyo wa chama cha
Republican, amekana kamwe hajawanyanyasa wanawake kingono, lakini akageuza
hasira kwa aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton katika majibizano makali
kwenye mjadala huo
"Hakuna mtu katika historia ya
siasa ambaye amewanyanyasa wanawake kiasi hicho," alisema.
Hillary Clinton alikataa kujibu
tuhuma hizo dhidi ya mumewe.
Matamshi ya bwana Trump dhidi ya
failia ya Clintons yalijiri baada ya muendesha mjadala Anderson Cooper
kumuuliza kuhusu kanda ya video ya mwaka 2005 iliyosambazwa katika vyombo vya
habari Ijumaa iliyomfichua Trump akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika
sehemu zao za siri.
Lakini alipoendelea kuulizwa kuhusu iwapo alimnyanyasa
kingono mwanamke yoyote, alikana kufanya hivyo na badala yake akamulika tuhuma
zilizomuandamana Bill Clinton katika siku za nyuma.
Hakuna mashtaka ya uhalifu
yaliowasilishwa dhidi ya Bwana Clinton katika tuhuma zozote z unyanyasaji wa
kingono.
Wagombea hao wawili bila walizozana
kuhusu mzozo wa Syria, Uchokozi wa Urusi, na hatua ya bwana Trump kukata
kutangaza malipo yake ya kodi na mpango wake wa ukaguzi mkali kwa wahamiaji
wanaowasili kutoka mataifa yanayohusishwana ugaidi.
Hatimaye mjadala ulikamilika wakati
mwanamume mmoja kutoka umati uliokusanyika kufuatilia mjadala huo, alipowauliza
wagombea hao wawili kusema kitu kimoja kizuri kumhusu mwenzake.
Mgombea wa chama cha Democrat
Hillary Clinton akasema watoto wake Trump wanamdhihirisha ni mtu wa aina gani.
Naye Trump akamtaja mpinzani wake
kuwa "mpiganaji" asiye kata tamaa.
No comments:
Post a Comment