1. Chura wakubwa Zaidi duniani wanapatikana nchini Cameroon barani
Africa na wana urefu wa futi moja na wamepewa jina la Golliath.
2. Africa ni bara la pilli kwa ukubwa duniani na hujumuisha
asilimia 22 ya ardhi ya dunia.
3. Africa ina makabila yapatayo 3,000. Na Nigeria pekee ina
makabila Zaidi ya 370.
4. Africa ndio sehemu yenye wanyama wakubwa Zaidi waishio ardhini,
ambao ni tembo na wanauzito kati ya tani 6 hadi 7.
5. Moja kati ya vyuo vikuu vikongwe Zaidi ulimwenguni hupatikana
Timbuktu Africa na kilianzishwa karne ya 12.
6. Mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania ndio mlima wenye kilele
kirefu Zaidi Africa, una urefu wa mita 5,895 kutoka katika usawa wa bahari.
7. Mto nile ndio mto mrefu Zaidi duniani, una urefu wa kilometa
6,670 na hupita katika nchi za Tanzania, Uganda, Sudani na Egypt.
8. Nusu ya almasi dunia hutoka kusini na katikati mwa bara la
Africa.
9. Ziwa Victoria ndio ziwa kubwa Zaidi barani Africa na ni ziwa la
pili kwa ukubwa duniani kwa maziwa yasiyo na maji chumvi.
10. Ziwa Nyasa ndio ziwa pekee lenye aina nyingi za samaki kwa
maji yasiyo na chumvi duniani.
No comments:
Post a Comment