Kim Kardashian
amepata mshirika wa kumsaidia kuwawinda majambazi waliomvamia na kumshikilia
kwa mtutu wa bunduki Jumatatu hii na kumuibia mali za thamani kubwa.
Si
mwingine, bali ni Rais wa Ufaransa, François Hollande.
Watu waliokaribu na staa huyo,
wanadai kuwa baada ya tukio hilo la Paris, Hollande yeye mwenyewe anahusika
katika uchunguzi na ameahidi kutoa ulinzi wa ziada kwa Kim mara nyingine akiwa
nchini humo, kwa mujibu wa Pagesix.
Kutokana na tukio hilo kuteka habari
za wiki hii dunia, mamlaka za Ufaransa zitaabika iwapo zitashindwa kuwakamata
watu hao watano waliokuwa wamefunika sura zao na Hollande anataka watu maarufu
akiwemo Kardashian, kurejea na kujihisi wako salama Paris.
Wakati huo huo, kuna taarifa kuwa
anatafutwa mtu anayefanana na Kim ili kumtumia kuchanganya watu na kumhakikisha
usalama zaidi kila anapotoka nje.
Pia watoto wake, North na Saint,
watakuwa na timu yao ya ulinzi kwakuwa Kim ana wasiwasi kuwa wao pia wanaweza
kutekwa. Kutokana na tukio hilo Kanye anadaiwa kumuonya mke wake kutomuamini
mtu yeyote ndani ya timu yake.
No comments:
Post a Comment