Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa na abiria aliyekuwa kwenye
shirika la ndege la Southwest Airlines.
Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake,
iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore,
Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa
Jumatano.
Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za
Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo
kwenye betri zake.
Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.
"Tunashirikiana na maafisa wa serikali na maafisa wa
shirika la Southwest kupata simu hiyo na kuthibitisha chanzo (cha moto
huo)," kampuni hiyo imesema kupitia taarifa.
Msemaji mmoja wa shirika la Southwest Airlines amemabia BBC:
"Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwa simu.
Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege."
Mmiliki wa simu hiyo Brian Green, akizungumza na Jordan Golson
wa shirika la The Verge, amesema alinunua simu hiyo tarehe 21 Septemba.
Amesema simu hiyo ilikuwa na alama ya mraba ya rangi nyeusi
kwenye pakiti yake, alama ambayo iliongezwa na Samsung kutofautisha kati ya
simu zilizokuwa zimeuzwa awali ambazo zilidaiwa kutokuwa salama na simu mpya
zilizokuwa zimechunguzwa.
No comments:
Post a Comment