Viongozi zaidi wa juu wa chama cha Republican, wamejiondoa kumuunga
mkono mgombea urais wa Marekani wa chama hicho, Donald Trump baada ya maneno ya
dharau aliyoyasema dhidi ya wanawake miaka 10 iliyopita kuvuja.
Zaidi
ya viongozi 10 wa chama hicho wamesema hawatampigia kura Trump tangu kauli hiyo
isambae kuanzia Ijumaaa. Trump anasema katu hatojiondoa kwenye kinyang’anyiro
hicho na kwamba hatowaangusha wafuasi wake.
Amekuwa kwenye kiti moto tangu
video ya mwaka 2005 kuvuja akisikika akiongea kuhusu kuwabusu wanawake na
kuwashika sehemu zao za siri.
Viongozi wa Republican waliojiondoa
kumuunga mkono ni pamoja na mgombea wa zamani wa kiti hicho John McCain na
waziri wa zamani mambo ya nje, Condoleezza Rice.
McCain amesema kauli ya Trump
inafanya ishindikane kumuunga mkono kwenye harakati zake. Naye Bi, Rice
amesema: “Enough! Donald Trump should not be President. He should withdraw.”
Seneta wa New Hampshire, Kelly
Ayotte amesema kwenye maelezo yake: I cannot and will not support a candidate
for president who brags about degrading and assaulting women.”
Mke wa Trump, Melania naye alitoa
maelezo Jumamosi akisema: The words my husband used are unacceptable and
offensive to me.” Hata hivyo alimtetea akidai kuwa mumewe ana moyo na fikira za
kiongozi.
No comments:
Post a Comment