Watu 17 wauawa Myanmar - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 10 October 2016

Watu 17 wauawa Myanmar

Watu 17 wameuawa nchini Myanmar wakiwemo Polisi
Vikosi vya usalama nchini Myanmar vimesema kuwa watu 17 wameuawa wakiwemo polisi tisa, mauaji hayo yametokea katika kituo cha polisi huko katika mpaka wa nchi hiyo na Bagladesh

Afisa mmoja wa Polisi amewaambia waandishi wa habari kuwa miongoni mwao ni washambuliaji wanane ambao waliuawa wakati wa mapambano katika jimbo la Rakhine.
Imeelezwa kuwa washambuliaji wawili walikamatwa.
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na jamii ndogo ya kiislamu ya Rohingya.
Kumekuwa na mvutano mkali katika Jimbo la Rakhine kati ya jamii ya Budha na jamii ya kiislamu ya Rohingya.

Shambulio la hivi karibuni linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea jimboni Rakhine tangu mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here