Vyoo vyote vya wanawake na wanaume
vinapaswa "kuwa salama, safi, na vinavyofaa" kuwabadili watoto
ubinda.
Sheria hiyo iliyopewa jina Vyoo
vinavyopatikana katika hali zote (BABIES) iliwasilishwa mara ya kwanza mnamo
Aprili na mbunge David N Cicilline.
"Mijengo ya serikali
inafadhiliwa walipa kodi," anasema.
"Ni muhimu kuhakikisha kwamba sehemu hizo zipo wazi
zinapatikana, na zenye kujali maslahi ya familia iwezekenavyo."
Sheria hii inafanya maenoe hayo ya
umma "kujali maslahi ya baba na mama wanaofanya kazi" kote Marekani.
Hakuna sheria maalum Uingereza
kuhusu meneo ya kuwabadili watoto ubinda, Raymond Martin, mkurugenzi wa British
Toilet Association (BTA) anasema.
Shirika hilo liliundwa miaka 20
iliopita kupiganiavyoo bora vya umma nchini.
Wakati huo, anakadiria kuwa ni choo
kimoja kati ya vyoo kumi vya wanaume vilikuwa vimetengewa nafasi ya kuwabadili
watoto ubinda na kuwafanyia usafi. HIvi sasa ni zaidi ya thuluthi mbili.
"Hili ni jambo lililopuuzwa," ameiambia BBC.
"Tumekuwa tukishirikiana na
mashrika mengi na kampuni kubwa za utengenezaji bidhaa wanaotufuata kwa ushauri
na muongozo."
Lakini anishutumu serikali,
akieleza kuwa 'hazitaki kuwajibika' katika kuhakikisha Uingereza ina sehemu za
kutosha.
Na mojawapo ya wasiwasi mkuu,
Martin anasema, ni kiwango cha vyoo vya umma vinavyofungwa katika miaka ya hivi
karibuni.

No comments:
Post a Comment