Wanasayansi wameonya kuwa wale ambao hupenda kujipiga selfie mara kwa
mara, wana hatari ya kuwa wapweke.
Wanadai
inaweza kuwa ni ishara ya kuwa na matatizo kwenye mahusiano yao au tatizo la
afya ya akili.
Wanaojipiga sana selfie wanaweza
kuwa watu wenye kasoro au wanaotafuta kuangaliwa, utafiti umesema. Watafiti
nchini Thailand, walifanyia tathmini wanafunzi 300 na kuangalia mara ngapi
huangalia picha walizojipiga wenyewe.
Washiriki hao ambao wengi walikuwa
wanawake, walikuwa na umri kuanzia miaka 21 hadi 24, walihojiwa kuangaliwa kama
walikuwa ni watu wa kujiamini, kutaka kuonekana, tabia ya kuwa wenyewe au
upweke.
Wengi wao walionekana kutumia
asimia 50 ya muda wao wa ziada katika simu zao au kwenye internet.
Wataalam wanaamini kuwa wanaume na
wanawake wenye upweke hupenda kuchukua zaidi selfie kutafuta kukubalika na watu
wengine.
No comments:
Post a Comment