Katika barua alioandika kwa gazeti
la The Times, Lord Rickets amesema kuwa ombi hilo lilifanywa mapema mno.
Ombi la kutaka ziara hiyo ya Donald
Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali limefaulu kupata zaidi ya saini milini
1.5.
Siku ya Jumatatu, maelefu ya watu
nchini Uingereza waliunga maandamano dhidi ya agizo la usafiri la Donald Trump
kuhusu mataifa saba ya kiislamu.
Mkakati huo wa uhamiaji wenye utata
ulizua mjadala bungeni.
Lord Rickets ambaye alikuwa katibu
wa maswala ya kigeni kutoka mwaka 2006-10 alisema kuwa sio jambo la kawaida kwa
rais wa Marekani kualikwa kwa ziara ya kitaifa katika mwaka wa kwanza wa
utawala wake.
Alihoji iwapo bw Trump alistahili
heshima hiyo .
''Ingekuwa vyema kusubiri na kuona
ni kiongozi wa aina gani kabla ya kumshauri Malkia kumualika.Sasa Malkia
amewekwa katika hali ngumu sana'',aliongezea kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment