Senegal yaingiza vikosi vyake Gambia - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 20 January 2017

Senegal yaingiza vikosi vyake Gambia

Gambia
Vikosi vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barroe anaapishwa.
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye ameiambia BBC kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,Banjul.Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.

Mapema baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh.Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.
Mpaka sasa haijafahamika wazi lini lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here