Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria umeangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa.
Jeshi la Syria lilisema kuwa ndege yake ya kijeshi ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi la Islamic State wakati ilishambuliwa siku ya Jumapili.
Imesema kuwa kisa hicho kitakuwa cha athari katika vita dhdi ya ugaidi.
Marekani ilisema kuwa ilichukua hatua za kujilinda baada ya serikali ya Syria kuangusha mabomu karibu na wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani.
Kisa hicho kilitokea mji wa Ja'Din ambao unashikiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF).
Wapiganaji wa SDF wanaoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Marekani wamezingira ngome ya IS huko Raqqa.
Saa mbili kabla ya ndege hiyo kuangushwa, Marekani ilisema kuwa vikosi watiifu kwa raisi wa Syria Bashar al-Assad viliwashambulia wapiganaji wa SDF na kuwajeruhi kadha.
Mapema mwezi huu, Marekani iliangusha ndege isiyo na rubani ya seriikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia vikosi karibu na kivuko cha mpaka cha al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.
No comments:
Post a Comment