Habari inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile
Audio (voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na
Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa
kimapenzi.
jana kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM Mbowe ameielezea
sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka:
“Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka
zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu
ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.
“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo
limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli
utajulikana tu muda sio mrefu.
"Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii
kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni
taarifa za upotoshaji tu."
No comments:
Post a Comment