Mimi ni La Familia niliyeishi Wasafi kwa muda – Chid Benz - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 23 June 2017

Mimi ni La Familia niliyeishi Wasafi kwa muda – Chid Benz


Msanii wa Bongo Fleva, Chid Benz amefunguka ni kwa nini sasa hivi hafanyi kazi na Babu Tale kama ilivyokuwa kipindi alichotoa ngoma yake ‘Chuma’ aliyomshirikisha Rayvanny ambapo alionekana kuwa karibu zaidi na lebo ya Wasafi.

Rapper huyo amedai kuwa kabla ya kuanza kufanya kazi na Babu Tale tayari alikuwa na project zake alizotaka kuzifanya lakini Tale kuna vitu alitaka kuongeza kwake hivyo project zake zikasimama lakini baadae walikuja kushindwana.
“Niliamua nifanye na Tale kwa sababu ana nafasi fulani anaweza kunifikisha sehemu lakini tumeenda na nafikiri alikuwa ananipenda sana akasahau kuna vitu alikuwa anatakiwa na mimi kunivumilia, ni vitu ambavyo vinanijia kwenye dunia ya sasa hivi. Mimi nilikuwa kwenye game kabla ya Tale, amenikuta kwenye game wasanii wengi waliokuwa Tip Top wengi walikuwa La Familia, nilikuwa nawasimimia, kwa hiyo yeye alitakiwa anisamimie pia. Sijawahi kusema amekosea, amepatia kwa upande wake lakini kwa upande wangu angenivumilia,” Chid Benz amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM na kuongeza.
“Tale asingetakiwa kuachana na mimi, angenichukulia kama mdogo wake, asikae anitangaze kwenye media kwamba amenishindwa. Sikuwahi kuwa Wasafi, nilikuwa La Lamilia ambaye ninayeshinda Wasafi na kufanya kazi Wasafi. Kitu watu hawakielewi ile ngoma yangu ilipigwa nembo ya Wasafi na mwisho unasikia ‘Laizer’, Laizer ni prodyuza wa Wasafi sijui alifanya nini labda mixingi lakini mimi najua track aliifanya T Touch,” amesistiza Chid.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here