Shirika moja la ndege la kibinafsi nchini India limemtuku safari za bure mtoto aliyezali ndani ya moja ya ndege zake, iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea nchini India.
Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto umbali ya futi 35,000 angani.
Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi wa Mumbai.
Shirika hilo liliiambia BBC kuwa mama na mtoto wake walikuwa katika afya nzuri.
Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.
Shirika hilo lililisema kuwa ndiyo mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege yake.
Lakini mashirika kadhaa yamekumbanana hali kama hiyo. Wahudumua wa shirika la ndege la uturuki wallisherehekea kuzaliwa kwa mtoto msichana ndani ya ndege mwezi Aprili mwaka huu.
No comments:
Post a Comment