Tufanye ‘Amendment’ ya sheria marais wote waweze kushtakiwa- Lijualikali - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 14 June 2017

Tufanye ‘Amendment’ ya sheria marais wote waweze kushtakiwa- Lijualikali

  Tokeo la picha la lijualikali bungeni
Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Lijualikali, jana bungeni ameshauri bunge liweze kufanya mabadiliko ya sheria ili liweze kuondoa kinga ya Rais ili ma-Rais wote waliofanya makosa waweze kushtakiwa kisheria kama watu wengine.

Lijualikali amesema hayo jana bungeni wakati akitoa maoni yake baada Rais Magufuli kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa madini na kusema wao kama wabunge wameshajua ACACIA ni wezi kwa mujibu wa ripoti hiyo aliyokabidhiwa na Profesa Osoro.
Akiishauri serikali amependekeza kinga ya rais iweze kuondolewa ili waweze kushtakiwa kama watu wengine pindi wanapofanya makosa, akidai kuwa haiwezekani Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Wizara husika akafanya maamuzi juu ya madini pasipo Rais kufahamu lolote.
“Rais ameshasema kuwa watu waliohusika wafanyiwe kazi, lazima bunge liondoe kinga ya Rais, tufanye ‘Amendment’ hapa Bungeni marais wa nchi hii wasiwe na kinga ya kutoshtakiwa, kwa sababu hainiingi akilini leo unamwambia Nazir Mustafa Karamagi, huwezi kuniambia mzee wangu huyu Chenge kwamba ahojiwe lakini marais waliopita wanaachwa haiwezekani Chenge afanye makosa rais asijue, haiwezekani baraza lilikuwa halijui. Tufanye ‘Amendment’ ya sheria marais wote waweze kushtakiwa” alisema Lijualikali.
Hata hivyo Lijualikali alisisitiza kuwa vita hii ya madini inapaswa kuwa vita ya taifa zima na si kuwa vita ya mtu mmoja mmoja na kudai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kuomba radhi kwa wananchi kutokana na hasara ambayo nchi imepata kwa viongozi wake kusaini mikataba mibovu inayolitia taifa hasara kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here