Waziri Nchemba Radhi Sakata la Walemavu Kupigwa na Jeshi la Polisi - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 20 June 2017

Waziri Nchemba Radhi Sakata la Walemavu Kupigwa na Jeshi la Polisi


Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu.

Mwigulu Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili siku nyingine lisijirudie.

"Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie" alisema Mwigulu Nchemba

Mnamo tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here