Marekani kuipa Ukrain silaha za kupambana na waasi - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 25 July 2017

Marekani kuipa Ukrain silaha za kupambana na waasi

Ukrainian President Petro Poroshenko meets servicemen during a visit to Donetsk region in June
Mjumbe mpya wa Marekani nchini Ukrian anasema kuwa Marekani inatathmini ikiwa itatuma silaha kusaidia wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na Urusi.

Kurt Volker aliiambia BBC kuwa kuihami serikali ya Ukrain itabadilisha msimamo wa Urusi.
Alisema hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi.
Wiki iliyopita wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Marekani ilizitaka pande zote mbili kusitisha mapigano mashariki mwa Ukrain.
"Silaha za kujilinda, zile ambazo zitaisaidia ukrain kujilinda na kuharibu vifaru kwa mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukrain," bwana Volker aliiambia BBC.
Alisema kuwa mafanikio ya kuwepo amani mashariki mwa Ukrain yanahitaji kile alichokitaja mchakato wa mazungumzo na Urusi.
Bwana Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye Nato na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 wameuawa tangu mzozo wa Mashariki mwa Ukrain ushuke mwezi Aprili mwaka 2014 mara baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea.
Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here