STAA kiwango kunako filamu Bongo, Kajala Masanja kwa mara ya kwanza ametokwa povu kuwa hakuna kitu ambacho anakichukia katika maisha yake kama mtu kumbambikia kiki ambazo zinahusiana na kutembea na mume wa mtu au bwana wa mtu kwa sababu haimjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.
Akizungumza na Ijumaa, Kajala, alisema kuna watu wengi wako radhi kutengeneza kiki kama hizo za kuchukuliana mabwana lakini kwake hazitaki na zinamkera sana kwa sababu mambo hayo yameshapita na wakati na kwanza pia hayamjengei chochote kwenye jamii zaidi ya kumuharibia.
“Kiki kama hizo sizitaki kabisa kuzisikia kwanza zinaniharibia wala hazinijengi chochote kwenye jamii yangu zaidi ya kuniletea picha tofauti kwenye jamii yangu,” Kajala alitoa povu.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Friday, 22 September 2017
Home
Unlabelled
Kajala Awatolea Povu Wanaomsema Anatoka na Mume wa Mtu
Kajala Awatolea Povu Wanaomsema Anatoka na Mume wa Mtu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment