Msanii wa bongo fleva na mama wa mtoto mmoja Linah Sanga ameibuka na kusema akibeba mimba nyingine hataacha kupiga picha zake tata kama alizozipiga kipindi akiwa na mimba yake ya kwanza kwa kuwa yeyeni mtu maarufu.
Akiongea kupitia eNewz Linah amesema hajutii kwa picha alizozipiga katika kipindi cha ujauzito wake wakwanza kwa kuwa yeye ni mtu maarufu na aliamua kufanya kitu ambacho roho yake ilijisikia kufanya kwa kipindi kile na kuongeza kwamba hata siku akibeba mimba nyingine anaweza kufanya kitu kama hicho kwa kuwa hakikumuharibia chochote katika maisha yake.
Hata hivyo Lina aliendelea kusema kwamba "Binadamu ni watu wa ajabu sana na hata ufanye nini huwezi kuwaridhisha kwa kuwa kila mtu anatamani ufanye kile anachokitaka yeye nikivaa gauni refu watasema mimi nimshamba na hata nimevaa hizo nguo fupi bado wanasema hazina maadili hivyo mi nafanya ninachojisikia na waacha waendelee na malumbano yao"alifunguka mbele ya kamera za eNewz
Mbali na hayo Linah amefafanua pia suala la watu kumuona yeye kama amechelewa kujifungua ni kutokana na kwamba watu wengi waliwahi kufahamu hali yake mapema tangu ikiwa na miezi mitatu hivyo walikuwa kama wanamuhesabia na ilipopitiliza wiki ndipo walipoanza kuhoji.
Facebook Twitter Google+ Pinterest Linkedin
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Wednesday, 20 September 2017
Home
Unlabelled
Linah Adai Hatoaacha Kupiga Picha za Utata Akibeba Mimba Tena
Linah Adai Hatoaacha Kupiga Picha za Utata Akibeba Mimba Tena
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment