Mwili wa mtoto ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa siku moja umeokotwa kwenye mfereji wa kupitisha maji machafu katika eneo la Mtaa wa Ali Nyanya kata ya Ungalimited jijini Arusha.
Kichanga hicho kimeonekana kutekelezwa na mama yake mzazi mara tu baada ya kujifungua na kupelekea kupoteza maisha, baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamelaani kitendo hicho cha kinyama na kikatili kinachofanywa na baadhi ya wanawake wasiokuwa na hofu ya Mungu ndani yao ambao wanakatisha uhai wa watoto hao ambao hawana hatia.
Mwenyekiti wa Mtaa huo Omari Shehe naye amelaani kitendo hicho na kuahidi kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha wanamtafuta muhisika ambaye amefanya tukio hilo la kinyama ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hizo za kufanya uovu na ukatili huo.
Vitendo vya watu kutekeleza watoto vimekuwa vikishamiri katika maeneo mbalimbali ya nchi huku wengi wakionekana kufanya ukatili huo kutokana na baadhi ya wanaume kukataa watoto au ujazito jambo ambalo hata hivyo halikubaliki.
No comments:
Post a Comment