Mchekeshaji wa kundi la Timamu Africa, Ebitoke amesema ameamua kumuacha Ben Pol aliyekuwa akidaiwa kuwa mpenzi wake kipindi cha nyuma.
Kauli ya Ebitoke inakuja mara baada ya drama za hapa na pale hivi karibuni kuwa wawili hao wamezinguana licha ya wao kutopenda kuliweka hilo wazi. Akizungumza na Papaso ya TBC Fm Ebitoke amesema kutokana na ubize wa Ben Pol na malengo yake ameamua kumuacha.
“Unajua mapenzi ni hisia, nahisi nilikuwa kama namlazimisha lakini nimegundua siwezi nikakosa furaha nikashindwa kufanya baadhi ya malengo yangu, kwa hiyo nimeamua kumuacha afanye maisha yake, ameniacha na mimi nimemuacha tu, nimeamua kutulia nifanye mambo yangu” amesema Ebitoke.
Katika hatua nyingine amesema kwa sasa hawezi kuja kumtangaza mpenzi wake hadharani na kitu alichojifunza ni kukaa kimya katika maisha ya kimahusiano.
No comments:
Post a Comment