Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili Msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’ Oktoba 19, 2017.
Lulu anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Msanii mwenzake, Steven Kanumba bila kukusudia kinyume cha kifungu cha 195 cha kanuni za adhabu (PC), April 7/2012 nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu, kesi ya Lulu itaanza kusikilizwa siku ya Oktoba 19/2017 mbele ya Jaji Sam Rumanyika.
No comments:
Post a Comment