LICHA ya mastaa wenzake akina Shamsa Ford na Aunt Ezekiel kuwatolea povu wasichana wanaowamendea waume zao, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ yeye ameibuka na kudai hana hofu hiyo, kwani anamwamini mpenzi wake, kama anavyojiamini mwenyewe.
Akizungumza na Za Motomoto News, Shilole alisema yeye na mpenzi wake Uchebe wanaaminiana na mapenzi yao wamemkabidhi Mwenyezi Mungu na kwamba mwandani wake huyo ni mtu wa dini hivyo ni vigumu kumsaliti.
“Sihofii kuibiwa Uchebe wangu maana namwamini na yeye ananiamini hata ninapokuwa safarini nje ya nchi huwa sina hofu maana ni mtu wa dini na mume wangu hana mambo ya wanawakewanawake kabisa, mapenzi yetu tunamtanguliza Mungu zaidi maana kwa akili zetu hatuwezi,” alisema Shilole.
Stori Na Gladness Mallya
No comments:
Post a Comment