Video: Nimekuja Dar kwaajili ya Danube sio Diamond – Zari - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 16 October 2017

Video: Nimekuja Dar kwaajili ya Danube sio Diamond – Zari


Mama watoto wa Diamond, Zari The Bosslady ametua jijini Dar es salaam jioni ya leo akitokea nchini Afrika Kusini kwaajili ya kuzindua duka jipya la bidhaa za nguo, Danube.




Mrembo huyo ametua katika Uwanja wa JK Nyerere International akiwa bila mtoto wake mdogo Nillan kitendo ambacho kimeonyesha huwenda mrembo huyo ajafika kwaajili ya Diamond na ni kwa muda mchache.

Akiongea na waandishi wa habari muda mchache baada ya kuwasili, Zali alisema amekuja nchini kwaajili ya uzinduzi wa duka la Danube sio kitu kingine

“Nimekuja Tanzania kama balozi wa Danube sio Diamond. Kwahiyo nashukuru kwa upendo wetu, na tuendelee kutumia bidhaa za Danube,” alisema Zari.

Zari amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Mlimani City jijini Dar es salaam siku ya kesho kwaajili ya uzinduzi wa duka hilo.

Wawili hao waliingia kwenye mgogoro mzito wa mapenzi baada ya Diamond kuchepuka na mwanamitindo, Hamisa Mobetto na kufanikiwa kupata mtoto mmoja. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here