Wasaliti CHADEMA Kunyofolewa Viungo - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday 12 October 2017

Wasaliti CHADEMA Kunyofolewa Viungo


Diwani wa kata ya Sombetini Arusha Ally Bananga (CHADEMA) amewataka madiwani waliopo ndani ya chama chao wanaotaka kuhama ndani ya chama waondoke mapema kwani wakija kuwagundua kipindi cha uchaguzi kwamba ni wasaliti watawatawanya viungo.

Bananga amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya wimbi la madiwani Arusha kuhama chama hicho kwa tuhuma za kupokea rushwa, ambapo ameweka wazi kwamba anaamini kwamba hakuna tatizo la madiwani kuhama vyama kwani ni uhuru kama ilivyo kwa mashabiki wa simba kwenda Yanga kwa ajili ya maslahi yao lakini wasiondoke kwa kununuliwa kwani haitakuwa busara na mwisho wa siku itakuwa ni matatizo.

"Sina tatizo kwa madiwani kuhama hata kidogo. Lakini kama ni kuhama kwa kununuliwa kama hivi tunavyoona hili ni tatizo. Kama huna imani  ondoka mapema kwa amani. Tupishe kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi na tunaamini tutashinda kata zote,  sasa isije ikatokea mbeleleni tukakugundua kwamba wewe ni msaliti maana tutatawanyana viungo kitu ambacho siyo kizuri. Ondokeni kwa amani yote sasa hivi mapema" - Bananga.

Aidha Bananga amesema kwamba amesikia maneno yaliyozungumzwa na aliyekuwa Diwani wa Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi na kueleza kwamba hawezi kumsemea neno baya kwani ni rafiki yake lakini pia amemtaka  asifanye madhabahu ya Mungu kama kaunta ya 'bar' kwani ni mtu anayemfahamu na wanajuana ni mangapi wamefanya pamoja hivyo asijisahaulishe.

"Namheshimu sana Ngowi. Lakini amekubali kufika bei mimi nilishajua siku nyingi na nilimwambia. Hata watu waliokuwa wakiongea naye waliniambia. Ametafuta laana ya Mungu, yeye anajiita Mchungaji jambo ambalo nina wasiwasi nalo. Lakini kwa maneno aliyoyasema kwenye mkutano Soko kuu lakini ndiyo ameshanunuliwa, Mungu siyo mjomba yake na Madhabahu asiigeuze kama kaunta." Bananga ameongeza

Ameongeza kwamba "Adhabu ya Mungu inamfuata kabla ya adhabu yetu sisi Chadema tutakayompatia wakati atakapogombea. Kama yeye ni mwanaume asogeze pua yake kwenye uchaguzi huu mdogo aone tutakavyomfanya".

Pamoja na hayo Bananga amesema anaamini ushindi katika uchaguzi mdogo lazima watashinda kwani wamekuwa bora chini ya uongozi wa Mbunge Godbless Lema na Meya Calist Lazaro na kutokana na ushahidi wa Nassari kuonyesha wabunge walikuwa wakinunuliwa kama maandazi safari wamejiandaa kupeleka keki kwenye chaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here