Na Anitha Jonas – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi katika mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini wenye lengo la kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo masuala ya kiimani, kijamii na kiuchumi.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Hajjat Shani Kitogo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
“Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1999 Sura ya Nane inazungumzia Malezi na inasema mafunzo ya dini yatakuwa sehemu ya malezi ya watoto ili kusisitiza Maadili,Malezi Mema, Kazi, Kustahiana na Kuvumiliana,” alisema Hajjat Kitogo.
Akiendela kuzungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi huyo alisema serikali inatambua umuhimu wa Viongozi wa Dini katika ulezi wa jamii na maendeleo ya Taifa na ndiyo maana imeona ni vyema kukutana nao na kujadili ni namna gani itaweza kulisimamia taifa katika kufikia malengo.
Naye mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bi Hadija Kisubi alitoa maoni yake na kusema anaamini viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kujenga nidhamu ya kwa taifa sababu ya neema ya mungu iliyondani ya viongozi hao pale wanatoa maelekezo kwa umma.
Pamoja na hayo mkutano huo umebeba Kauli Mbiu inayosema “Imani na Uzalendo Kuelekea Uchumi wa Viwanda” na utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) tarehe 25/10/2017.
No comments:
Post a Comment