Mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mustafa Hassanali, ameonekana kwenda kinyume na matakwa ya mwanamitindo wa kiume bongo Calisah, akisema kuwa kijana huyo sio mwanamitindo kabisa
Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mustafa Hassanali amesema kama Calisah angekuwa mwanamitindo mwenye sifa angeshafanikiwa kwenda kwenye majukwaa ya mitindo kimataifa, lakini kwa kuwa hana sifa, hata ya hapa nyumbani ameshindwa kufanikiwa kupanda.
Mustafa ameendelea kwa kusema kwamba tasnia ya mitindo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, na kama huna nidhamu basi hakuna utakalofanikisha.
"Calisah sio model, acha ugomvi uanze, unajua London fashion week, Heriet Paul alifanya Victoria secret ambayo ilifanyika Shangai, kama unajiita super model mbona Swahili Fashion hayupo? Kila mtu ana maisha yake na anataka kuishi jinsi anavyotaka, asiyefundishwa na mamaye hufundishwa na nani? Kama mtu hawezi kurespet na kuthamini biashara ya ubunifu, huwezi fanikiwa", amesema Mustafa Hassanali.
Kitendo cha mwanamitindo huyo kutolewa sifa na watu walioko kwenye tasnia yake imekuwa ni mara ya pili, ambapo awali mwanamitindo Dax Cruzz alisikika akisema Calisah hana vigezo vya kuwa mwanamitindo wa kimataifa na kwamba ataishia hapa hapa bongo.
No comments:
Post a Comment