Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ijumaa hii limeonya kuhusu kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, likisema kuwa serikali inafaa kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha mwelekeo wa kushuka.
Katika taarifa yake mpya kuhusu uchumi wa Tanzania, IMF imesema kuwa, licha ya kuwa takwimu za pato la taifa kuoyesha kukua, lakini takwimu ningine za uchumi zinaeleza kudorora kwa shughuli za kiuchumi. Taarifa hiyo imetolewa baada ya kukamilisha mapitio yake ya Sera za Kukuza Uchumi PSI kuhusu Tanzania.
Ukusanyaji wa mapato umekuwa mdogo kuliko ulivyotarajiwa na ongezeko la alama za imani limekwama katika baadhi ya mabenki kutokana na kuongezeka kwa mikopo mibaya.
Kumekuwa na athari mbaya kwenye ukuaji wa uchumi katika kipindi kifupi kutokana na utekelezaji mdogo wa bajeti, ulioleta changamoto kwenye mazingira ya kibiashara, na sekta binafsi ikilalamika kubanwa sana na sheria.
Uchumi wa Tanzania katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka, lakini mwezi Novemba Benki ya dunia ilitangaza kuwa kasi hiyo huenda ikapungua hadi asilimia 6.6 mwaka jana
No comments:
Post a Comment