Msimamo mpya wa Rais kuhusu kunyonga watu - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, 21 January 2018

Msimamo mpya wa Rais kuhusu kunyonga watu

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anatafakari uwezekano wa kuanza tena kuwanyonga wahalifu nchini humo.

Rais Museveni amesema licha ya kwamba yeye ni "Mkristo" kuwa dini yake imemzuia kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wale ambao wamehukumiwa kunyongwa, hata hivyo amesema, hali hiyo imekuwa ikiwatia moyo wahalifu.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kuhitimu kwa askari wa idara ya magereza, katika gereza la Luzira jijini Kampala ambapo ni miaka 13 sasa tangu Uganda ilipotekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu.

Watetezi wa haki za kibinadamu wameshutumu tamko hilo la Rais Museveni na kusema adhabu ya kifo haikomeshi uhalifu.

Mara ya mwisho kwa Rais Museveni kuidhinisha hukumu ya kifo itekelezwe ilikuwa katika gereza la Luzira mwaka 1999 na mwaka 2005 aliidhinisha mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya kifo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here