Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga pamoja na familia zao wamesherehekea Sikukuu ya Familia‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’ kwa ajili ya kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.
Sikukuu hiyo imefanyika Jumamosi Januari 6,2018 katika uwanja wa michezo wa mgodi wa Bulyanhulu uliopo kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu.
Akizungumza wakati wa kusherehekea sikukuu hiyo,Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu alisema lengo la sikukuu hiyo ni wafanyakazi na familia zao kujumuika pamoja kufurahia mwisho wa mwaka uliopita na kujitayarisha kwa ajili ya mwaka mpya 2018.
“Katika kusherekea sikukuu hii tumeialika jamii inayotuzunguka kujumuika nasi kwa ajili ya kuonesha upendo,tunaonesha pia shughuli tunazofanya,vikundi vya wajasiriamali vinavyozunguka mgodi ambao tumekuwa tuvikiviwezesha kutengeneza bidhaa mbalimbali ambavyo vitakuwa na ushindani mkubwa katika masoko,tuna imani mwaka huu utakuwa na mafanikio makubwa”,alieleza Busunzu.
Busunzu alisema hivi sasa mgodi umeanza shughuli za uzalishaji lakini uzalishaji umepungua kutokana na matatizo yaliyojitokeza mwaka 2017 na kuongeza kuwa wataendelea kutekeleza miradi waliyokuwa wameahidi kuifanya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kuendelea na utamaduni wa kuandaa sikukuu ya familia kwani wamekuwa wakiwakutanisha wafanyakazi wa mgodi na jamii inayowazunguka.
“Shughuli hizi za kukutanisha watu pamoja zinajenga jamii,nimekuwa nikihudhuria sikukuu hizi,mwaka jana nilihudhuria pia sikukuu ya familia katika mgodi wa Buzwagi,na hakuna tatizo lolote linalotokea,niwapongeze sana kwa kuunganisha jamii”,alieleza Nkurlu.
Katika kusherehekea sikukuu hiyo,mbali na washiriki kula,kupata vinywaji,kucheza pia shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo maonesho ya mitambo inayotumika kuchimbia madini katika mgodi huo,maonesho ya vikundi vya wajasiriamali wanaozunguka mgodi huo,utoaji damu,utoaji wa zawadi kwa watoto na burudani mbalimbali zikiongozwa na kundi la sanaa la Mrisho Mpoto 'Mjomba team'.
Uongozi wa mgodi huo,pia umetumia fursa hiyo kukabidhi mabati 64 na matofali zaidi ya 2900 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Beya iliyopo katika halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita ambayo hivi karibuni majengo yake yalibomoka baada ya mvua kubwa kunyesha.
Tanzama picha za tukio zima hapomchini
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akielezea lengo la Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’ Jumamosi Januari 6,2018 katika uwanja wa michezo wa mgodi huo-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akizungumza wakati wa Sikukuu ya Familia
Mtaalamu wa Mawasiliano mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi, Mary Lupamba akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sikukuu ya Familia ya mgodi wa Bulyanhulu
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Sikukuu ya Familia mgodi wa Bulyanhulu mwaka 2018 ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kutambulishana
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’
Keki maalumu kwa ajili ya Sikukuu ya Familia ya Bulyanhulu
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akikata keki,kushoto ni Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu
Mrisho Mpoto 'Mjomba' aliyekuwa MC mkuu katika sikukuu ya Familia ya Bulyanhulu mwaka 2018 akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ili aimbe live wakati wa sikukuu hiyo
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiongoza Live Band ya Mrisho Mpoto 'Mjomba'.Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni mlezi wa Mrisho Mpoto Live Band alionesha umahiri wake wa kuimba nyimbo mbalimbali ukiwemo wa Mario
Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu wakicheza muziki wakati mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akifanya yake live jukwaani
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiimba live jukwaani
Mtaalamu wa Mawasiliano mgodi wa Bulyanhulu na Buzwagi Mary Lupamba na mme wake wakicheza muziki wakati mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiimba live jukwaani
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akicheza na mtoto wake
Burudani inaendelea
Burudani ya muziki inaendelea
Kila mmoja na staili yake ya kucheza...
Kulia ni Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu (kulia) akionesha uwezo wake wa kucheza
Burudani inaendelea...
Michezo ya watoto ikiendelea wakati wa sikukuu ya familia
Mrisho Mpoto akiimba na kucheza na watoto
Watoto wakicheza muziki
Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu wakiangalia burudani ya muziki kutoka kwa watoto
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akiwa na familia yake
Mchekeshaji Oscar Nyerere akiigiza sauti za viongozi mbalimbali
Mchekeshaji Oscar Nyerere akiwa na Mrisho Mpoto wakati akiigiza sauti ya rais John Pombe Magufuli
Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu wakifurahia burudani ya Mchekeshaji Oscar Nyerere
Mcheza sarakasi kutoka kundi la Mrisho Mpoto akionesha uwezo wake wa kuruka juu
Hatari sana....Vijana kutoka kundi la sanaa la Mrisho Mpoto wakitoa burudani
Wanafamilia wakiwa eneo la tukio...
Kundi la burudani la Wakali Sisi kutoka Kakola wakitoa burudani
Tunafuatilia matukio yanayoendelea...
Wanafamilia wakifurahia jambo..
Zoezi la kuchukua vinywaji baridi likiendelea wakati wa sikukuu ya familia
Chakula nacho kilikuwepo cha kutosha,pichani ni foleni kuchukua chakula
Nyama choma nazo zilikuwepo
Wazazi wakiwasindikiza watoto kuchukua chakula
Zoezi la kula chakula likiendelea
Muda wa chakula.....
Kundi la sanaa la Mrisho Mpoto likitoa burudani
Burudani kutoka Kundi la Mjomba Mpoto ikiendelea....
Wanenguaji wa kundi la Mjomba balaa.....
Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu wakipiga stori eneo la tukio
Meza ya mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakifuatilia burudani kutoka kundi la Mrisho Mpoto
MC Ice kutoka Shinyanga akitoa maelekezo
Msanii God Four kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiimba wimbo
Zoezi la utoaji zawadi ya vifaa vya shule kwa watoto likiendelea
Watoto wakiangalia zawadi zao
Watoto wakiwa katika eneo la tukio
MC Mary Lupamba na Mc Ice wakifanya yao
Zoezi la utoaji damu kwa hiari likiendelea....
Muda wa kutembelea Vibanda vya wajasiriamali wanaoishi karibu na mgodi ambao wanawezeshwa na mgodi huo wa Bulyanhulu: Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiangalia CD kuhusu ufugaji kuku wa mayai ya kienyeji katika banda la kikundi cha ufugaji kuku cha Mamuu Chicken.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiangalia kuku
Kushoto ni Mzee Samwel Igoko akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu kuhusu mradi wao wa ufugaji wa nyuki na kumuonesha asali waliyotengeneza
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiwa katika banda la wakulima wa mboga mboga
Hapa ni katika banda la kundi la akina mama wanaotengeneza nguo na sabuni
Mama mtengeneza sabuni za maji akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu namna wanavyotengeneza na kuuza sabuni hizo
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiangalia mitambo inayotumika kuchimba madini ya dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu..Pichani ni mtambo unaotumika kama ngazi kufanyia kazi za juu
Huu ni mtambo unaotumika kuchoronga mashimo
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akimkabidhi kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'hwale Rajabu Mmunda bati moja kati ya mabati 64 yaliyotolewa na mgodi huo kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Beya ambayo majengo yake yalibomolewa na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni
Kushoto ni Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akimkabidhi kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'hwale Rajabu Mmunda tofali kati ya matofali zaidi ya 2900 yaliyotolewa na mgodi huo kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Beya iliyopo katika halmashauri ya Nyang'hwale
Bi Maida Waziri akizungumza wakati wa kuchangia shilingi 200,000/= kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Beya
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'hwale Rajabu Mmunda akiushukuru mgodi wa Bulyanhulu kwa kusaidia mabati na matofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Beya
Mfanyakazi wa Bulyanhulu bwana Terry Little akiwa amebeba nyoka na watalaamu kwa kucheza na nyoka kutoka kundi la Mrisho Mpoto
Mfanyakazi wa Bulyanhulu akiwa amebeba nyoka...
Burudani ya kucheza na moto ikiendelea...
Mtaalamu wa kucheza na moto kutoka kundi la Mrisho Mpoto akiweka moto kwenye kaptura yake.
Chanzo na Picha Malunde 1
No comments:
Post a Comment