WALIMU 28 WAFUKUZWA KAZI KWA KULAMBA SH MILIONI 100 - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 17 January 2018

WALIMU 28 WAFUKUZWA KAZI KWA KULAMBA SH MILIONI 100

       
Na Muhammed Khamis, Mwananchi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewafukuza kazi walimu 28 baada ya kugundulika kufanya ubadhirifu wa zaidi ya Sh100.4 milioni.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Mjini Zanzibar leo Jumatano, Katibu Mkuu Kiongozi, Abdul-Hamid Yahya Mzee amesema pamoja na kufukuzwa kazi walimu hao waliokuwa wakichukua mishahara hewa lakini pia wanatakiwa kulipa fedha hizo serikalini.

Amesema uamuzi huo umekuja baada ya uhakiki katika wizara mbalimbali za Serikali ya Zanzibar na kubaini kasoro ambazo watendaji wake walionekana kufanya makosa hayo kwa makusdi.

Amesema sababu za kufukuzwa kwa walimu hao ni kuchukua fedha za mishahara bila ya kuwepo kazini kwa muda mrefu huku wakishindwa kabisa kutoa taarifa kwa wahusika.

Mzee amesema kwa mujibu wa takwimu zao katika uchunguzi huo zinaonyesha watumisihi 46 wa Wizara ya Elimu visiwani hapa wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya kustahiki kulipwa fedha hizo.

“Kwa mujibu wa takwimu zetu zinaonyesha kuwa watendaji waliokosa kuripoti kazini kwa muda mrefu ni 20 wagonjwa 8 na 6 hawakujitokeza kabisa katika uhakiki huo huku wengine wakishikiliwa kwa makosa mbalimbali.’’

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here